Friday, April 29, 2011


19.    Draw me close


[1]
Draw me close to you,
Never let me go, 
I lay it all down again,
To hear you say that I am your  friend

You are my desire,
No one else will do,
Nothing else can
take your place,

To feel the warmth
of your embrace,
Help me find a way,
bring me back to you
[chorus]
You are all I  want
You are all
I’ve  ever needed,

You are all I  want
Help me know
you are near !

Help me know
you are near !

Tuesday, April 19, 2011

Jesus Loves us

A
He will come back to take us to New Jerusalem

Saturday, April 16, 2011

Unaijua siri iliyoko katika tabasamu?

*smile*
Unajua Siri iliyoko katika kutabasamu?
IN SMILE THERE IS LOVE
NDANI YA UPENDO LIMO TABASAMU 
Vipi wewe na umpendaye?
*  Kumjua mtu anayekupenda huburudika kukuangalia usoni kwako mda mrefu.
*  Ukiangaliwa tu, TABASAMU
1. Tabasamu hutufanya tuvutie
Smile makes us cerebrate

2. Kiafya Tabasamu huongeza mfumo wa kinga
Hufanya kinga kufanyakazi kwa spidi maana mwili umejiachia
3. Tabasamu huambukiza furaha kwa watu wengine.
TABASAMU KATIKA PENDO
4.Tabasamu hudumisha upendo na mapenzi.

5.Tabasamu hupunguza Mishtuko ya mwili-Stress 
Stress hutoweka pale tunapotabasamu na kuufanya mweli ujiachie huru 

6 . Tabasamu hupunguza Shinikizo la damu (Blood Pressure)
7. Tabasamu huachilia Endorphins (kituliza Maumivu cha asili) na Serotonin
SMILE HADI BASI
8. Tabasamu hunyanyua uso na kufanya UONEKANE BADO MDOGO. Maana yake ukinuna sura inakuwa kama m-bibi/m-babu 
KAMUA TABASAMU
SMILE FOR FUTURE
9. Tabasamu hufanya mtu awe na mtazamo chanya (positive mind)

Tuesday, April 5, 2011

ASKOFU MKUU TAG: Bora kufa kuliko kunywa mizizi ya Loliondo

 BORA KUFA KULIKO KUNYWA MIZIZI YA LOLIONDO

Askofu Mkuu TAG: Dr Barnabas Mtokambali
KATIKATI ya mahubiri yake mbele ya maelfu ya waumini na wachungaji, waliokusanyika katika kanisa la Gospel Campeign Centre Majumbasita, Kiongozi Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk. Barnabas Mtokambali, alionya kuwa kanisa ambalo ni mali ya Kristo limekwisha kunywa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani,
hivyo halihitaji kwenda Loliondo kunywa mizizi na wala halitanywesha watu wake. 

           Mtumishi huyo wa Mungu alitoa msimamo huo alipokuwa katika ziara ya kichungaji katika Section (sehemu) ya Ilala, Jimbo la Mashariki, ambapo maelfu ya waumini na viongozi wa kanisa hilo walifurika kumsikiliza.
Alisema kuwa Kanisa la TAG, ni mali ya Mungu, hivyo ni lazima lisikilize maagizo kutoka kwa mwenye mali, ambaye ni BWANA Yesu, na siyo kwa mwingine awaye yote.
“Kwakuwa TAG ni mali ya Mungu, ni lazima lifanye kazi katika viwango vya kimungu zaidi, lilinde utakatifu, na kutoa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu, yanayopingana na mafundisho potofu,” alisema Dk. Mtokambali na kuongeza:
          “Wakati umefika sasa wa kufanya mapinduzi makubwa ya kiroho na kumwambia shetani hapana. Mtu muovu aache uovu wake na amrudie BWANA.”
Kisha Dk. Mtokambali alisisitiza: “Yesu ni yeye yule jana na leo na hata milele; miujiza yake haijabadilika kamwe, tangu wakati alipoishi katika umbo la mwili hapa duniani na hata wakati wa Matendo ya Mitume, hakuwahi kunywesha watu dawa... wala kunywa dawa.        Tunachotakiwa kufanya ni kuendelea kumwamini tu, hata kama tunakufa, afadhali kufa na ugonjwa wako ufike mbinguni kuliko kunywa dawa na kuishia hapa duniani.”
        Alisema tangu nyakati za Yesu na hata wakati wa Matendo ya Mitume hakuna aliyetenda miujiza kwa kutoa dawa, hivyo kwakuwa kanisa la TAG limejengwa katika misingi ya kanisa la Matendo ya Mitume litaendelea kumtegemea Mungu, mtenda miujiza likifuata misingi halali ya Neno la Mungu, na siyo vinginevyo.
Huku akishangiliwa na waumini waliofurika katika ibada hiyo, Askofu Dk. Mtokambali, alisema,
TAG, itaendelea kusimamia msimamo wake wa kusimamia Neno la Mungu, na kulinda imani thabiti, bila kuyumbishwa na upepo wowote unaovuma na utakaovuma, haitakunywa dawa wala kugawa dawa kwa waumini wake, kwa kuwa Kiongozi wake Yesu Kristo, hakuwahi kufanya hivyo.
        Kwa wiki kadhaa maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika huko Loliondo kunyweshwa dawa na mchungaji mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwaisapile, inayodaiwa kuwa inaponya magonjwa sugu makuu matano.
Baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini wamekuwa wakimiminika katika eneo hilo kunyweshwa dawa hiyo, huku baadhi ya wagonjwa waliopelekwa huko wakipoteza maisha kutokana na mazingira magumu ya miundombinu, kukosekana kwa vyakula na maji safi.
Wakati tunakwenda mitamboni kulikuwa na taarifa za kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza, katika eneo hilo duni na baadhi ya viongozi wa dini wakijikuta katika utata wa kitheolojia.
Baadhi ya Wachungaji wamekuwa wakiwaruhusu waumini wao kunywa dawa, huku wengine wakiweka wazi misimamo yao kuwa dawa hiyo haikithi vigezo vya kiimani wala kuungwa mkono na Neno la Mungu aliye hai.
      Baadhi ya Wakristo, wamekuwa wakipiga simu kwenye Gazeti la Jibu la Maisha, kutafuata ushauri wa kiroho ikiwa ni halali kwa mtu aliyeokoka kuyweshwa dawa ya Babu wa Loliondo au laa. Huku wengine wakionesha wazi kuwa wamebaki dailema kutokana na ukimya wa viongozi wao wa kiroho.
     Akielezea sababu kuu ya kufanya ziara hiyo, Askofu Mkuu Dk Mtokambali, alisema kuwa hiyo ni moja ya utekelezaji wa kuunda kasi mpya ya Mpango Mkakati wa Miaka Kumi ya Mavuno, wenye lengo la kuivuna Tanzania, na kuikabidhi kwa BWANA Yesu, ambao umri wake ni miaka miwili sasa tangu kuzaliwa kwake, Octoba 2008.
Askofu Dk. Mtokambali, alitaja sababu kuu tatu ya ziara hiyo kuwa ni, kufanya ziara ya kichungaji, kuja kuwapongeza kwa kazi nzuri pamoja na kuwahimiza kuongeza bidii zaidi katika kuleta maendeleo ya kanisa na katika kuivuna Tanzania.
“Mchungaji mzuri ni yule anayewatembelea kondoo, na kujua hali zao; ujio wangu mimi ni wa kichungaji zaidi, nimekuja kuongea nanyi, kula na kufanya ibada ya pamoja ili sote kwa pamoja tujenge na kuboresha upya mpango mkakati wetu tuliouweka katika ubora zaidi na wenye kasi kubwa ndani ya mika hii minane iliyosalia,” alisema Askofu, na kuongeza:
“Nguzo kuu ya uchungaji ni kuwatembelea washirika, katika ziara zangu nchini, nimewaagiza Maaskofu wa Majimbo, Waangalizi na Wachungaji, kutokaa ofisini na badala yake watembelee watu na kujua shida zao,” alisema.
      Aidha alisema kuwa, endapo kanisa litazingatia na kutumia vyema rasilimali watu, fedha na vifaa mbalimbali walizo nazo wanaweza kutekeleza mpango huu mkakati ndani ya miaka sita tu na sio vinginevyo.
Dk. Mtokambali alifurahishwa sana na kutiwa moyo na kazi kubwa iliyofanywa na makanisa ya Sehemu ya Ilala, ambapo alisema takwimu zao za sasa zinaonesha kuwa, ndani ya miaka hiyo miwili idadi ya waumini wapya walioongezeka ni 1026, kati ya hao watu wazima 276, na watoto 750 na kufanya jumla kufikia waumini 8450, kutoka 7424, waliokuwepo awali.
Wakati huo huo, Sara Mushokolwa, anaripoti kuwa Mchungaji Godwin Mujaki, wa Kanisa la Ubungo Msewe, akihubiri katika Ibada ya Jumapili aliwaasa Wakristo kuachana na maji ya Loliondo, maana hayana tofauti na uganga wa kienyeji, yanaashiria tu kuwa hizi ni nyakati za mwisho ambazo ni za hatari na wateule wanapaswa kuwa makini sana.
Alisema kuwa huo ni kama upepo unaovuma kwa kasi hivyo ni vyema kuwa makini nao maana siku zote Biblia inasema miujiza huambatana na kumtukuza Mungu, na si kunyweshwa mizizi.
Hakuna kitu katika yale maji ya Loliondo, huo ni uchawi kama ulivyo uchawi mwingine, kwa kuwa maandiko matakatifu yanaeleza wazi kuwa maji ya uzima ni Yesu,” alisema Mchungaji Mujaki.
Naye Chanyika Zephania, anaripoti kuwa, Mchungaji Paulo Mulokozi wa Kanisa la Ubungo Christian Centre, ameitahadharisha jamii ya Watanzania wanaoridhia tiba ya Babu, Mch. Ambilikile Mwasapile, kuwa Mungu hayupo katika jambo hilo, tena hizo ni hila za shetani.
“Mungu hayupo katika jambo hilo, huo ni uharibifu na hatari kwa jamii yetu ya Kitanzania, hivyo ni marufuku kwa wanaonisikiliza, na iwapo unao ndugu wanaokwenda huko muwashauri wasiende,” alisema.
      Mch. Mulokozi alieleza kuwa kuna Sheikh maarufu, ambaye amewashauri waumini wake kwenda katika tiba hiyo, jambo linaloashiria kupingana na ukweli kiimani na haiwezekani uponyaji wa kimaombezi ya kweli kupata ushabiki kwa masheikh ambao kwa kawaida hupingana na maombezi yanayotumia Jina la Yesu.
      Mjadala mkubwa unaendelea miongoni mwa watanzania juu ya tiba inayoendelea huko kijiji cha Samunge Loliondo inayoendeshwa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile (Babu), huku Serikali ikiwa na kigugumizi kuhusu utafiti wa kitaalamu kuhusu dawa hiyo.