Tuesday, February 15, 2011

Heart of Worship: Listen and Read


  Heart of worship!

[1]
When the music fades,
all is triped away
And I simply come,

longing just to bring something
that of worth that will bless your heart
                       
I bring you more than a song
for the song in itself is not all that you have required

You search much deeper within
Through the way things appear
You are looking into my heart,
[chorus]
Am coming back to the heart of worship
It's all about you, Its all about you, Jesus

Am sorry Lord for the things I made,
It's all about you, its all about you Jesus.
[2]
King of endless worth
no one could express
How much you deserve,
though am weak and poor,
All I have is yours, every single breath.

It's all about you x2
It's all about you Jesus

Monday, February 14, 2011

Nini maana ya Siku ya Valentino

Asili: Jina la Mtakatifu wa Kiroma aliye itwa Valentino
Siku ya Mtakatifu Valentino- Siku ya wapendanao wanaiita “Valentine Day”, ni maadhimisho ya mwaka, kila tarehe 14 Februari, Watu husherehekea upendo na kuthaminiana na kujaliana kati ya watu wenye uhusiano binafsi, mara nyingi hutumika kwa mahusiano ya kimapenzi.

Siku hii asili yake ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwaajili ya kuupenda Ukristo.  Historia inasema Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia, Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga. Mtakatifu Valentino aliteswa kwaajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa tarehe 14 mwezi Februari, 269 AD. Kwaajili ya msimamo, imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza tarehe 14 mwezi wa pili kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.
Watu wanasherehekeaje siku hii?
Tuichukulie siku hii kidini zaidi. Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanawe kama kafara ya Dhambi zetu. Ni vizuri tukitumia mda tulio nao kujitakasa na kutubu dhambi zetu. Je sisi ni nini mbele za Mungu zaidi ya wale waliokuwa wanachinjwa na kuuawa kikatili kwaajili ya kulinda imani yao? HADI PUMZI YA MWISHO WALIMTAMKA KRISTO. Tuwaenzi kwa kutenda wema tu.
Namaanisha tupendane kwa upendo wa Kimungu, Upendo wa Kweli, Upendo wa Kiuaminifu. Siku hizi Upendo wa kweli ni Mgumu kwawatu wengi kwasababu mbalimbali, ikiwemo dhambi na anasa za kidunia. Swala la Uaminifu, Duh! Linapelekesha watu sana.
JAMANI TUSHEREHEKEE VALENTINE ILA TUSIIGEUZE NCHI YETU KUWA KAMA SODOMA NA GOMORA.
Biblia inasema kila tunapotenda dhambi moja Tunampandisha Yesu msalabani tena. MUNGU ATUSAMEHE
SEMA AMEN