Asili: Jina la Mtakatifu wa Kiroma aliye itwa Valentino
Siku ya Mtakatifu Valentino- Siku ya wapendanao wanaiita “Valentine Day”, ni maadhimisho ya mwaka, kila tarehe 14 Februari, Watu husherehekea upendo na kuthaminiana na kujaliana kati ya watu wenye uhusiano binafsi, mara nyingi hutumika kwa mahusiano ya kimapenzi.
Siku hii asili yake ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwaajili ya kuupenda Ukristo. Historia inasema Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia, Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga. Mtakatifu Valentino aliteswa kwaajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa tarehe 14 mwezi Februari, 269 AD. Kwaajili ya msimamo, imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza tarehe 14 mwezi wa pili kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.
Tuichukulie siku hii kidini zaidi. Mungu aliupenda ulimwengu na kumtoa mwanawe kama kafara ya Dhambi zetu. Ni vizuri tukitumia mda tulio nao kujitakasa na kutubu dhambi zetu. Je sisi ni nini mbele za Mungu zaidi ya wale waliokuwa wanachinjwa na kuuawa kikatili kwaajili ya kulinda imani yao? HADI PUMZI YA MWISHO WALIMTAMKA KRISTO. Tuwaenzi kwa kutenda wema tu.

Biblia inasema kila tunapotenda dhambi moja Tunampandisha Yesu msalabani tena. MUNGU ATUSAMEHE
SEMA AMEN
No comments:
Post a Comment